Thursday, November 8, 2018

MRADI WA MKAA MBADALA


UMOJA WA WALIMU WASTAAFU MKOA WA SHINYANGA kupitia kikundi chake cha BIO-MASS BRIQUETTERS wanakusudia kuanza ujenzi wa banda la kusimika mashine yao ya kuzalisha MKAA MBADALA (BIO-MASS BRIQETTES) kwa kutumia taka ngumu katika eneo la Viwanda, Ibadakuli Kitongoji cha Wilgwamabu,nyuma ya Kiwanda cha AHAM. UJENZI unaanza kwa kutumia pesa za michango ya Wanakikundi hao waliokubaliana kuunganisha nia zao ili kutoa mchango katika Hifadhi ya Mazingira na kuonesha FURSA za kiuchumi.

Monday, November 5, 2018

SHERIA HIZI ZINAHUSU NANI?

Nimeangalia kwa siku nyingi na nimeijiwa na hili wazo la leo, hivi hizi Sheria za usalama barabarani ni kwa ajili ya madreva wa magari tu? Mbona waendesha mapikipiki hawazifuati?
1. Kwenye zebra hawasimami,
2 Maeneo ya makazi hawafuati alama zilizowekwa
3. Ubebaji wa abiria nao ni mshikaki
4. Helmet hazivaliwi na dereva hadi abiria
5. Matumizi ya Low & High beam lights hayafuatwi usiku.
Yapo mengi na yanatendeka huku Matrafiki wakiyaona mbele yao lakini kwao si jambo la kipaumbele.
Hapo kunakuwepo na maswali mengi kuhusu usalama wa Raia na uhalali wa namna ambavyo Trafiki Ordinancy inavyosimamiwa.


WAHUSIKA HILI NALO LIONENI

Kama kweli imekusudiwa kuwawezesha wananchi wa kawaida kupata habari, basi hili la VISIMBUZI na APPS zinazotolewa na TV kv AZAM App,  STARTIMES App na nyinginezo,  litazamwe upya;
Mteja anaweza kupata habari na kuangalia michezo kupitia TV yake mwezi mzima kwa kulipia kifurushi kisichozidi Tsh.  20,000/= lakini asiye na TV akiamua kupata huduma hizohizo kupitia APP kwenye simu yake, Tsh. 20,000/= haitoshi hata siku 5.
Tungetegemea kundi hili la watu nalo likawezeshwa kupata huduma za TV kwa APP kwa gharama sawa na mtumiaji wa TV, gharama  ya pamoja na vifurushi vya Intaneti. Naamini hili linawezekana likiwekewa namna nzuri ya utekelezaji.
Vinginevyo App hizi hazina manufaa sana kwa wanaoziDOWNLOAD kwani matumizi yake ni Ghali mno.
WAHUSIKA LIONENI hili.


Tuesday, October 30, 2018

MASIMULIZI YA KIZUSHI

Mtu mmoja alipanda mti, mti wenye sifa ya kivuli na matunda na aliupanda kwa madhumuni hayo lakini hakuratibu ukuzaji wa mti huo.
Mara mti ulianza kusinyaa na kunyauka kwa ukame, yeye eti hakuwa na chakufanya kwa kuwa chanzo cha ukame ni Mapenzi ya Mungu.
Alisahau au hakutaka au hakujua kuwa mti huo ukimwagiliwa maji kwa makini katika kipindi chote cha ukame, ungechipuka na kuendelea kukua katika kipindi hicho kigumu cha ukame na hata kumpatia kivuli na matunda.
Hapa panakuja swali, kaupanda nani, lini, kwa ajili ya nani, wapi na kwa nini!
Japo mti, una gharama zake, japo mti, una thamani yake, japo mti, una sifa zake, japo mti, una madhumuni yake na japo mti, una watu wake, watu wake wakiuona unateketea, wanachomoa, wanatunza.
SASA, TUNZA UTUNZWE.
Monday, October 29, 2018

SHUKRANI ZETU

FAMILIA ya Mwl. Nsolo S. Stephen wa Bugweto_A, Shinyanga wanawashukuru Ndugu, Marafiki na wote popote waliojitoa kwa Hali na/au Mali KUFANIKISHA SEND_OFF ya Florentina Milabo Nsolo, Alhamis 25/10/2018  nyumbani kwa Mwl. Nsolo, Bugweto.
na USHUHUDA wa  NDOA  Jumamosi 27/10/2018 Bukene, Nzega.
TWAWASHUKURUNI SANA.
          © Mwl. Nsolo


Sunday, September 30, 2018

KUMHUDUMIA MAMANew YouTube Post

New YouTube Upload

KUMHUDUMIA MAMA

via IFTTT

Saturday, September 22, 2018

NI KILIO KIKUBWA KWA WATANZANIA

Kwa mara nyingine Tanzania tumepata pigo la kupoteza Roho za Watanzania wengi katika tukio moja la kuzama Kivuko cha MV. Nyerere lililotokea 20/09/2018 Ziwani Victoria huko Ukala wilayani Ukerewe.
Watanzania wengi kutoka familia nyingi wamefariki kwenye tukio hili,  Watanzania wengi kutoka Familia nyingi wamejeruhiwa, Nasi katika nafasi mbalimbali tumepata majeraha kwa kufiwa Watanzania wenzetu, Marafiki, Ndugu au Wanafamilia wetu. Hili ni janga linalotutonesha majanga mengine ya miaka si mingi iliyopita,  kuzama MV Bukoba, Kuteketea kwa moto Wanafunzi wa Shauritanga, Ajali ya Treni wilayani Mpwapwa,  Tetemeko la Bukoba, Dhoruba ya Mwakata Wilayani Kahama,  Makumi ya Wanafunzi kuangamia kwa ajali ya basi na mengine mengi zikiwemo ajali za mabarabarani zimechukua Roho nyingi za Ndugu zetu.
Tutumie muda huu kumwomba Mumgu Mwenyezi awape Marehemu wote Pumziko na Raha ya Milele, Mwanga wa Milele awaangazie,  wapumzike kwa amani. Tuwaombee majeruhi wote uponaji wa haraka.
Kwa njia yake na ndani yake,  tunaomba hayo,  AMENI.


Friday, September 21, 2018

WASIFU WA MAREHEMU JACKSON MASUNGANew YouTube Post

New YouTube Upload

WASIFU WA MAREHEMU JACKSON MASUNGA

via IFTTT

Put your email below, we will send Offers and new story notification

Like uweze kubahatika na zawadi tukitangaza